SERIKALI imepata zaidi ya Sh bilioni 1.3 katika mnada wa madini aina ya tanzanite yaliyokamatwa na kutaifishwa.
Mnada huo ulifanyika juzi wakati wa maonesho ya tano ya Kimataifa ya
madini ya vito na usonara jijini hapa na kusimamiwa na Mkurugenzi wa
Uthaminishaji wa Almasi na Vito kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Archard Karugendo.
Mnada mwingine uliofanyika katika maonesho hayo ulikuwa ni wa madini
ya tanzanite kutoka mgodi wa TanzaniteOne na Stamico, madini ambayo
yalikuwa hayajakatwa na yaliuzwa kwa zaidi ya Dola za Marekani milioni
2.2 (sawa na Sh bilioni 4.6). Karugendo alisema katika mauzo hayo ya
madini ya Tanzanite One, Serikali imepata mrabaha wa zaidi ya Sh milioni
245.
“Katika fedha hizo zilizopatikana kutokana na mauzo ya Tanzanite
kutoka mgodi wa TanzaniteOne, serikali itapata mrabaha wa zaidi ya Sh
milioni 245 na matokeo ya mauzo ya maonesho yote yatatangazwa na kamati
ya maandalizi ila haya ni matokeo ya madini yaliyouzwa kwenye mnada tu,”
alisema Karugendo Kaimu Kamishna wa Madini kutoka wizara hiyo, Ally
Samaje alisema mapato hayo yaliyotokana na mnada huo yanakwenda moja kwa
moja serikalini.
“Mapato yote hayo zaidi ya Sh bilioni 1.3 yanaingia serikalini, kwani
madini hayo yalikamatwa na kutaifishwa na yalikuwa chini ya serikali
tangu mwaka jana yalipokamatwa, “ alisema Samaje.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: