Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imetupilia kesi ya wakazi 2619 ya kupinga kubomolewa nyumba zao bila kulipwa fidia yoyote na serikali kwa wakazi zaidi ya elfu nne wa eneo hilo mara baada ya wakazi hao kukosa majina na sahihi za wananchi walioomba kuwakilishwa katika kesi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Jaji Fredrica Mgaya wakati shauri hilo amesema kesi hiyo imefutwa kwa kukosa majina na sahihi za watu wanaotaka kuwakilishwa na watu wanane walioshauliana kuwa watawasimamia katika kesi hiyo ya bomoabomoa ya wakazi wa jimbo la Segerea.
Akisoma maamuzi ya wakili wa serikali Gabriel Malata amesema kuwa walalamikaji hawana kibali au viapo halali vya wakazi hao kuomba kuwakilishwa na watu walioteuliwa kuwasimamia katika kesi yao ya kubomolewa makazi yao.
Pia Jaji Fredrica Mgaya ameiomba serikali kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni ili wajue athari zitakazowakuta kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: