ads

ASILIMIA 26 ya hisa zilizokuwa zinamilikiwa na mbia mwenza wa serikali, katika kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre Arusha, zimenunuliwa na serikali na hivyo kiwanda hicho kwa sasa kinamilikiwa na serikali kwa asilimia 100.


Hayo yalibainishwa jana bungeni na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM).

“Je, ni lini serikali itafungua rasmi kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre ambacho kilikuwa mkombozi kwa uchumi wa taifa na kilichotoa ajira kwa wananchi wa Arusha?” Alihoji Magige.

Mwijage akijibu alisema serikali imeweka dhamana ya kusimamia na kuendesha kiwanda hicho, chini ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kwamba tangazo la Serikali (GN) kuhusu uamuzi huo litatolewa wakati wowote kuanzia jana.

Alisema dhamira ya serikali ni kuona kiwanda hicho kitaanza kuzalisha matairi mapema iwezekanavyo na tayari wizara imeagiza NDC kuandaa andiko la kitaalamu, ambalo pamoja na kujibu masuala ya kiuchumi.

Pia shirika hilo litatoa majibu ya kiufundi na kijamii na kwamba ni lazima lizingatie maoni ya wadau wa sekta husika kwa ajili ya kuboresha kiwanda hicho. Aidha, mradi huo utaendeshwa chini ya menejimenti ya rasilimali watu wenye weledi katika biashara ya matairi na bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini.

Awali kiwanda hicho kiliacha uzalishaji mwaka 2009 baada ya serikali kukosa fedha za kukiendesha huku mbia mwenza kampuni ya Continental AG, kutokuwa tayari kuendelea na uwekezaji huo. 



DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: