WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewasili
nchini kutoka Kampala, Uganda na kusema miundombinu ya Tanzania na
usalama wake ni moja ya mambo yaliyowezesha Tanzania kupata dili la
ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi bandari ya Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili jana
jioni alisema kwamba maunganiko ya reli ya Tanga hadi reli ya Kati na
uwapo wa barabara kumeipatia Tanzania nafasi ya ujenzi wa bomba hilo
kwani kaskazini mwa Kenya miundombinu hiyo haipo.
Akizungumza huku akimfagilia Rais John Magufuli kwa kazi yake nzuri
ya kusimamia ujenzi wa barabara wakati alipokuwa Waziri wa Ujenzi,
alisema kama kungelikosekana miundombinu hiyo kungeliikosesha Tanzania
mradi huo muhimu Afrika Mashariki.
Tanzania ilikuwa inashindana na Kenya katika kupata nafasi ya
kutekeleza mradi huo wenye kilomita 1,403 utakaobeba mafuta ghafi kutoka
Hoima nchini Uganda hadi Tanga. Mradi huo wa dola za Marekani bilioni 4
sawa na Sh trilioni 8.7 ni ushindi mkubwa kwa Watanzania ambao
walipeleka Uganda timu ya wataalamu kuwezesha ushawishi wa kwa nini
Bomba hilo la mafuta linafaa kupitia Tanzania.
Kwa mujibu wa Waziri Muhongo mradi huo utakamilika Juni 2020 na
kwamba mkutano wa Mawaziri wa Tanzania na Uganda wa Nishati na Madini na
wataalamu wao kuhusiana na mpango wa utekelezaji utafanyika Ijumaa
ijayo mjini hapa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: