ads

Crystal Palace itakutana na Manchester United katika fainali ya kombe la FA mwaka 2016, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Watford City.


Yannick Bolasie aliongoza Palace kabla ya Troy Deeney kusawazisha kunako dakika ya 55, lakini Conor Wickham alifunga bao la pili na la ushindi kwenye dakika ya 61.

Hiyo ni fainali ya kwanza kwa Palace katika kipindi cha miaka 26 kwenye kombe la FA, tangu ilipofungwa na Manchester United mwaka 1990.

Manchester United ilitinga fainali ya FA hapo jana baada ya kuifunga Everton mabao 2-1, kwa mabao ya Anthony Martial na Marouane Fellaini, huku Everton wakipata bao la kufutia machozi baada ya beki wa Manchester United Chris Smalling kujifunga.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: