Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema
kuwa wizara yake haitawavumulia watendaji wazembe na wasiotaka kuendana
na kasi ya serikali ya awamu ya tano.
Profesa
Mbarawa ametoa kauli hiyo alipotembealea makao makuu ya Mamlaka
ya Hali ya Hewa nchiniTanzania (TMA) na kubainisha kuwa anawataka
wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao
kikamilifu na kuwatendea haki watanzania ambao kwa kiasi kikubwa
wanawategemea wao kujua masuala mbalimbali yahusuyo hali ya hewa.
Aidha, Profesa Mbarawa amesema kuwa anaitaka mamlaka hiyo kuanzisha utaratibu wa kupima utendaji kazi wa wafanyakazi kwa mwaka mzima ambapo ndio kitakuwa kigezo cha kumpandisha daraja mfanyakazi au kumuongezea mshahara.
Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa ameitaka mamlaka ya hali ya hewa nchini kuachana na mfumo wa zamani wa kuhifadhi kumbukumbu zao kwa njia ya makaratasi na badala yake watumie njia ya komputa njia ambayo ni rahisi na inabana matumizi ya karatasi.

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: