ads

Msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz ameoneshwa kustushwa kwake na taarifa za kifo cha mwanamuziki mwenye asili ya Congo Papa Wemba, huku akielezea jinsi walivyokutana siku chache zilizopita na kufanya naye collabo.


Kwenye ukurasa wake wa Facebook Diamond ameelezea huzuni hiyo, huku akitoa taarifa kuwa kulikuwa na mipango mingi ya wao kufanya kazi, lakini mauti yameshafuta mipango hiyo.

“Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halafu ghafla naskia habari ya msiba...Dah! nimesikitika sana. Hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyez Mungu ndiyo mpangaji...Pumzika salama Kiongozi wetu daima tutakukumbuka” aliandika Diamond Plutnums kwenye ukurasa wake wa facebook

Msanii Papa Wemba amefariki dunia jana baada ya kuanguka akiwa jukwaani akiimba na kufariki papo hapo nchi Ivory Coast.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: