MACHO na masikio ya wananchi yameelekezwa leo bungeni kusikia jinsi
Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na
Walemavu inavyowasilisha makadirio ya bajeti.
Sambamba na hilo, pia hati nyingine itakayowasilishwa bungeni leo ni
Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2014/15 , ambapo
serikali itatakiwa kutoa majibu ya hoja mbalimbali za ukaguzi huo.
Bajeti hiyo inawasilishwa na Waziri Jenista Mhagama ikiwa ni wizara
ya kwanza kati ya wizara 18 za Serikali ya Awamu ya Tano ambayo wabunge
watajadili kwa siku tatu. Wizara ya hiyo inayoshughulika na masuala
nyeti ya kijamii kama vile wabunge, vijana, kazi na ajira, inategemewa
kuwasilisha bajeti itakayoonesha mpango wa kuboresha programu za kukuza
fursa mbalimbali za makundi yaliyo kwenye wizara hiyo.
Hivi karibuni, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alimkabidhi Rais
John Magufuli Sh bilioni 6, fedha ambazo Bunge lilisema zimetokana na
wao kujibana na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Hata hivyo vyombo vya habari mbalimbali juzi na jana viliripoti
baadhi ya wabunge wa bunge hilo wakilalamika kutolipwa mishahara yao ya
miezi kadhaa ya ubunge wao katika Bunge lililopita na kohoji iweje Bunge
liseme wana fedha ambazo wameona hazina matumizi ya maana.
Hilo pamoja na mengine ni baadhi ya mambo ambayo leo katika bajeti ya
wizara inayopendekezwa yanayoweza kuibuka katika mjadala wakati wa
uchangiaji hotuba ya wizara hiyo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: