RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya
mwaka 2014/15 iliyotolewa jana mjini hapa inaonesha kuwa kati ya vyama
22 vya siasa nchini vyenye usajili wa kudumu, ni chama kimoja pekee
ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa ajili ya ukaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Profesa Mussa
Asaad alitaja Chama cha Wananchi (CUF) , ndicho kimewasilisha hesabu
zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari mwaka 2015 hadi Juni
mwaka huo.
Alisema vyama vingine 21 vimeshindwa kufanya hivyo hali ambayo
amemshauri Msajili wa vyama hivyo kufuatilia jambo hilo.
“Ripoti hii
inabainisha kwamba vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni 22,
lakini hadi Juni mwaka 2015, vyama vilivyowasilisha hesabu zao kwa
ukaguzi ni chama kimoja tu cha CUF, sasa hivi vingine vimekiuka sheria
ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992”, alisema Profesa Asaad.
Akizungumzia udhaifu mwingine ambao umebainika katika ripoti hiyo
Profesa Asaad aliweka hadharani Balozi mbalimbali za Tanzania nje,
Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
Post A Comment: