ads

Kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kuwasili kesho kikitokea nchini Tunisia ambapo wamemuacha winga chipukizi wa Klabu hiyo Farid Mussa ambaye kesho anatarajia kuelekea nchini Uhispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.


Afisa habari wa Azan FC Jaffery Iddy Maganga amesema, Farid atakuwa huko kwa takribani mwezi mmoja na atafanya majaribio katika timu za Malaga na Las Palmas zinazoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo na atarejea jijini Dara es Salaam Mei 19 mwaka huu msimu wa ligi ukiwa umeisha. 

Maganga amesema, kwa upande wa kikosi cha Azam kitakachowasili kutokea nchini Dubai ambapo kilipitia kikitokea nchini Tunisia hakitaingia kambini bali kitaunganisha safari kuelekea jijini Mwanza ambapo kitapumzika kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho Tanzania 
Bara dhidi ya Mwadui ya mjini Shinyanga utakaopigwa Aprili 24 mwaka huu mjini Shinyanga.

Maganga amesema, kwa upande wa kocha wa kikosi hicho Stewart Hall mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ratiba jinsi ilivyopangwa lakini kikosi kimeshaandaliwa kwa ajili ya kuweza kufanya vizuri katika mchezo huo.

Azam FC itakuwa ugenini dhidi ya Mwadui huku Yanga ikiwa pia ugenini Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ikicheza dhidi ya Coastal Union.
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: