ZAIDI ya Sh milioni 320 zimetumika kulipia mishahara kwa wafanyakazi hewa wa serikali katika mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainika kutokana na uhakiki uliofanywa ikiwa ni utekelezaji
wa agizo la Rais John Magufuli kuwataka wakuu wa mikoa kuwabainisha
wafanyakazi hao.
Yalibainishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka alipotoa
taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake kutokana na kumalizika
uhakiki wa watumishi wa serikali mkoani hapa.
Alisema siku 15 zilizokuwa zimetolewa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa
Mikoa kuhakikisha wanawabainisha na kuwaondoa wafanyakazi hewa,
zimeonesha katika mkoa huo kuna wafanyakazi hewa 62 ambao wanapokea
mishahara hewa kwa vipindi tofauti.
“Tumebaini watumishi 62 kwa mchanganuo huu, watumishi 33 hawapo
kazini kabisa na 29 ni watoro kazini kwa kipindi kirefu. Wengine hadi
kufikia miezi 40 na wamekuwa wakipokea mishahara kama kawaida,” alisema.
Alisema kugundulika kwa watumishi hao hewa ni sawa na asilimia 0.5 ya
watumishi wote katika mkoa huo kwani hadi sasa una watumishi wapatao
13,174 huku akisisitiza ya kuwa Idara ya Elimu ndiyo iliyoongoza kuwa na
watumishi hao.
Post A Comment: