JESHI la Polisi katika Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya mkoani Mara,
linawasaka watuhumiwa watano wanaotajwa kuhusika kubaka wasichana wawili
katika eneo hilo.
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Andrew Satta alisema, watu hao
wanatuhumiwa kuwabaka wasichana hao katika matukio mawili tofauti
yaliyotendwa kwa nyakati tofauti Machi 26, mwaka huu katika wilaya za
Rorya na Tarime.
Satta alisema kuwa, katika tukio la kwanza mwanafunzi wa shule ya
msingi Kibasisi iliyopo kwenye kijiji cha Kangariani wilayani Tarime
(Jina limehifadhiwa), alibakwa na watu wawili wakati akirejea nyumbani
kutoka shuleni siku hiyo ya Machi 26.
Kamanda Satta alisema kuwa, mwanafunzi huyo alikutana njiani na watu
wawili waliokuwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni, ambao walimkamata
kwa nguvu, kumburuza vichakani na kumbaka kwa zamu. Alieleza zaidi kuwa,
baada ya kumbaka, watu hao walimdhibiti asipige kelele kwa kumfunga
kitambaa mdomoni.
“Walipomaliza kumbaka walitokomea kwenye vichaka na kutorokea mahali
pasipojulikana, lakini Polisi inawasaka,” alisema na kuongeza kuwa,
tukio hilo liliripotiwa Polisi na mwanafunzi huyo.
Post A Comment: