HATIMA ya Yanga kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Shirikisho la
TFF (FA) inatarajiwa kujulikana leo baada ya kikao cha Kamati ya
Mashindano kukutana.
Mechi ya nusu fainali kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa
kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita ilivunjika
katika dakika ya 110 baada ya wachezaji wa Coastal kukataa bao la pili
la Yanga na kuanzisha vurugu zilizosababisha mshika kibendera namba
mbili Charles Simon kupasuliwa jicho la kushoto kwa jiwe lililotupwa na
shabiki.
Kaimu Mkurugenzi wa mashindano wa
TFF, Jemedari Said alisema wanasubiri ripoti ya Kamisaa na mwamuzi ndipo
watoe maamuzi. “Jambo kama hilo likishatokea ni lazima kamati ya
mashindano ikutane, kuangalia sheria na kanuni zinasemaje kabla ya kutoa
maamuzi,” alisema.
“Taarifa tayari tunazo, ripoti zote zinatarajiwa kuwasilishwa ofisini
leo hii (jana) na kisha kamati chini ya Mwenyekiti Geofrey Nyange
‘Kaburu’ itakutana haraka iwezekanavyo kuamua,” alisema Said.
Katika mechi hiyo Coastal Union iliyoonesha soka safi ilipata bao la
kuongoza kupitia kwa kiungo wake Youssouf Sabo na Yanga ilisawazisha
kupitia kwa mshambuliaji wake Donald Ngoma.
Dakika 90 za mechi hiyo zilimalizika bila kupata mshindi na ndipo
ilipoamuliwa timu ziende muda wa nyongeza wa dakika 30, ambapo dakika za
mwanzoni tu Amisi Tambwe aliifungia Yanga bao la pili na ndilo
lililozua kizaazaa, ambapo Coastal ilidai Tambwe alifunga kwa mkono.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: