UMILIKI wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa Jiji la Dar es
Salaam, umekoma rasmi baada ya Kampuni ya Simon Group kukamilisha malipo
ya ununuzi wa hisa za jiji hilo katika shirika hilo ambazo ni asilimia
51.
Kutokana na kukamilika kwa malipo hayo, sasa Uda inamilikiwa Kampuni
ya Simon Group yenye asilimia 51 ya hisa ambazo ndizo zilizokuwa hisa za
Jiji na Serikali yenye asilimia 49.
Akizungumza Dar
es Salaam jana,
Msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru alisema mpaka katikati ya Aprili,
mwaka huu, Kampuni ya Simon Group ilikuwa imemaliza kulipia malipo ya
hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na Jiji.
Kwa mujibu wa Mafuru, sasa Serikali inapaswa kuitambua Kampuni ya
Simon Group kuwa mwenye hisa katika shirika hilo, kwa kuwa kampuni hiyo
imewasilisha nyaraka za ununuzi wa hisa hizo na Jiji limethibitisha
kupokea fedha zao na kukubali kwamba muamala huo wa malipo ni halali.
Akifafanua namna ununuzi huo ulivyo halali, Mafuru alisema Jiji
walifungua kesi kuomba mahakama iagize Kampuni ya Simon Group ilipe
fedha za hisa za Jiji kufikia Aprili 30 mwaka huu, kinyume cha hapo hisa
hizo zirudishwe kwa Jiji la Dar es Salaam.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: