Waziri wa Nishati wa Uganda Bi. Irene Muloni pamoja na timu ya
wataalamu wa wizara yake wapo nchini kwa ajili ya mkutano wa kwanza wa
majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta linalotarajiwa
kujengwa kutoka nchini humo hadi jijini Tanga.
Bomba hilo
litakalojengwa kwa ushirikiano baina ya serikali za Uganda na Tanzania,
awali lilikuwa lipitie nchini Kenya na litakuwa likisafirisha mafuta
ghafi kutoka eneo la magharibi mwa Uganda mahali ambako imegundulika
hazina kubwa ya nishati ya mafuta.
Mwenyeji wake, Waziri wa
Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospeter Muhongo amewaambia
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuwa mbali ya bomba la
mafuta, mkutano huo unaohusisha wataalamu kutoka nchi zote mbili,
utajadili pia ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Tanzania
kwenda nchini Uganda.
Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, bomba la gesi
litatumika pia kupeleka nishati hiyo katika mikoa ya kanda ya ziwa, kwa
kutumia michoro na miundombinu itakayopita kwenye eneo lile lile ambako
bomba la mafuta litajengwa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: