Sakata la wamiliki wa Makampuni yanayo simamia uendeshaji wa mradi wa
mabasi yaendayo kasi unazidi kuibuwa mapya mara baada ya halmashauri ya
jiji kukana kutambua kampuni ya Simon Group ambao wanadai kuwa na ubia
katika mradi huo.
Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wa Meya wa jijini la
Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita, Mjumbe wa Baraza la Halmashauri kuu ya
jiji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ubungo Mhe. Said kubenea amesema
Halmashauri ya jiji haijauza hisa zake kwa Simon Group na kumtaka
mmiliki wa Kamapuni hiyo kukimbilia Mahakami kwani mchakato wake haukuwa
halali.
Mhe. Kubenea amesema ni vyema Serikali ikaingilia kati kuondoa utata
huo ambao usiposhugulikiwa mapema utaligarimu taifa kutokana na kampuni
ya Simon Group kukopa fedha nyingi katika taasisi za kifedha hapa nchini
kwa ajili ya kuendesha mradi huo ambao usipofanikiwa utaangusha uchumi
wa taifa.
Aidha kubenea ameiomba serikali kuu kuingilia kati sakala hilo ambalo
linazidi kuwa na sintofahamau baada ya mchakato wake kugubikwa na
udanganyifu mwingi ambao unalipotezea taifa mabilioni ya fedha nakwamba
mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti ya CAG izingatiwe.
Naye Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amesema mchakato wa
kurudisha vitega uchumi vya mapato ya jiji umefika na kuwa ameunda
kamati mbili kuchunguza mradi wa machinga Coplex, kuhakiki makusanyo
katika soko la kariakoo, UDA, ikiwa pamoja na kuongeza makusanyo ja jiji
kutoka Bilioni 11.7 mpaka bilioni 20 kwa mwaka.
Akiongelea kamati hizo Meya amesema, maeneo muhimu yatakayo angaliwa
nipamoja na makusanyo katika soko la Kariakoo, Maduka yanayozunguka eneo
la shuke ya Benjamin Mkapa,Machinga Complex, shirika la usafiri la Dar
es salaam UDA.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: