Serikali ya Tanzania imesema itawasilisha muswada wa sheria katika bunge
utakaohakikisha kuwa watoto wote wanaosoma shule za msingi na sekondari
hawatasitisha masomo yao kutokana na ndoa za utotoni.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe, leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Ileje Mhe.
Janeth Mbene aliyetaka kujua ni lini serikali itafanya marekebisho wa
sheria ya ndoa nchini.
Dkt. Mwakyembe amesema kuwa mswada huo pia utaleta mabadiliko katika
sheria ya elimu ambapo itafanya watoto wote wa shule za msingi na
sekondari waweze kufaidi matunda ya sera ya elimu bure kwa wote hususani
kwa watoto wa kike.
Aidha ameongeza kuwa Wizara pamoja na tume ya kurekebisha sheria
imepanga kulifanya zoezi la ukusanyaji wa maoni kuhusu sheria ya ndoa na
sheria nyingine za wanawake kwa kuwafikia wanawake wengi zaidi kwa
kutumia mfumo wa White paper.
Dkt. Mwakyembe amesema kuwa kutokana na mchakato wa kuundwa tume ya
mabadiliko ya Katiba mpya, mchakato wa kufanya marekebisho ya sheria ya
ndoa na mapendekezo ya kutungwa kwa sheria mpya ya mirathi na urithi
ulisitishwa kwa muda ili kupisha ukusanyani wa maoni ya katiba mpya.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: