RAIS John Magufuli amekamilisha kutengeneza muundo wa serikali yake
na anatarajiwa kutangaza muundo huo katika Gazeti la Serikali (GN) muda
wowote kuanzia sasa.
Kutokana na kukamilika kwa muundo huo, Rais ameshatoa maelekezo ya
utendaji kwa mawaziri wote na viongozi wengine kulingana na muundo wa
serikali yake na hivyo wanatekeleza majukumu yao kutokana na maelekezo
ya Rais.
Hayo yalisemwa bungeni mjini hapa jana na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alipokuwa anatoa majumuisho ya hotuba ya bajeti ya Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017.
Waziri Mkuu alisema baada ya kuapishwa, Rais alianza kazi ya kuunda
serikali yake kwa kuteua mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wengine,
kazi aliyoendelea kuifanya hadi hivi Aprili 20, mwaka huu
alipoikamilisha.
Alisema tofauti na magazeti la kawaida, GN hutolewa baada ya
kukamilika kujengwa kwa hoja juu ya suala husika na ndio maana
isingekuwa vema kwa Rais kutoa tangazo hilo wakati akiendelea kuunda
serikali yake.
“Napenda sasa kuliarifu Bunge kuwa Rais atatangaza kwenye GN muundo
wa serikali yake wakati wowote kuanzia sasa, na kwa maana hiyo Mawaziri
wote na viongozi wengine wa juu wa serikali wanafanya kazi kwa maelekezo
ya Rais, lakini pia kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya CCM,” alisema
Waziri Mkuu Majaliwa.
Hoja kwamba serikali iliyopo madarakani haipo kihalali kutokana na
kutotangazwa kwa muundo wa serikali katika Gazeti la Serikali,
iliibuliwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman
Mbowe, na kusema ni moja ya sababu zilizoifanya kambi hiyo kususa hotuba
hiyo ya Waziri Mkuu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: