MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Simon Kagoli
amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuhifadhi wahamiaji haramu nyumbani
kwake na kuwatumikisha mashambani.
Kagoli ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kageji, anakabiliwa na
mashitaka matatu ikiwemo kuishi na watu ambao sio raia, kuwasaidia raia
wa kigeni kutenda kosa na kuajiri na kuwatumikisha wageni shambani
mwake. Kesi hiyo namba 114/2016 iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya
ya Kibondo, Robert Male.
Mwendesha Mashitaka wa Uhamiaji, Richard Mwangole alidai mshtakiwa
alitenda kosa hilo kwa makusudi huku akijua kuwa kuhifadhi wahamiaji
haramu ni kosa kubwa
. Anatuhumiwa kuwafanyisha kazi wahamiaji hao na
kuwalipa ujira wa Sh 110,000 kila mmoja. Male alikana makosa na yuko nje
kwa dhamana.
Alidhaminiwa na wadhamini wawili, kila mtu kwa dhamana ya Sh milioni moja.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: