MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema
Serikali italazimika kuchukuwa uamuzi mgumu katika kukabiliana na watu
waliojenga nyumba bila ya vibali na bila uzingatiaji wa taratibu za
ardhi.
Alisema uamuzi huo utahusu zaidi maeneo yaliyowekwa kwa ajili ya
miradi ya kijamii, vianzio vya maji pamoja na mitaro ya kupitishia maji
ya mvua.
Alitoa agizo hilo kwa masheha wote wa wilaya mbili za Magharibi
“A” na “ B” akiwataka kuanza kuorodhesha nyumba zote zilizojengwa bila
ya kibali na katika maeneo yasiyostahiki.
“Tunakusudia kubomoa majengo yote yaliyojengwa bila ya kibali na
kwenye maeneo ya njia za maji, ikiwa ni mwanzo wa uamuzi mgumu
utakaochukuliwa na Serikali,” alisema Balozi Seif.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: