KWA mara ya kwanza aliyekuwa Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, amezungumzia kutumbuliwa kwake
kulikofanywa na Rais Dk. John Magufuli, kuwa ni kawaida kihistoria na
haoni ajabu juu ya hilo
Balozi
Sefue aliyasema hayo wakati akizungumza jijini Dar es Salaam
juzi baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwatunuku vyeti vya shukrani
wadau mbalimbali wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, akiwamo Balozi Sefue,
vilivyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
“Kama unajua ilivyo kwenye historia, kwa kawaida marais wakishaingia madarakani, wanakuwa na Katibu Mkuu Viongozi waliowakuta kwa kipindi cha mpito, lakini baadaye wanakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi wa kwao, kwa hiyo siyo jambo la ajabu kwangu,” alisema.
Alipoulizwa juu ya maisha ya uraiani, alisema: “Hayo wakati wa kuyazungumza bado…kuhusu majukumu mengine nikipangiwa mtayasikia.
” Balozi Sefue aliteuliwa kuendelea na nafasi hiyo Desemba 30, mwaka huu, baada ya kuitumikia wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Dk. Jakaya Kikwete.
Kuhusu utendaji kazi wa Serikali ya Rais Magufuli, alisema: "Inafanya kazi nzuri sana na kwamba Watanzania wanapaswa kujiona wenye bahati. Mtu yeyote ambaye anaitakia nchi hii mema, hawezi kuacha kukiri kwamba chini ya uongozi wa Dk. Magufuli, tumeona mabadiliko makubwa yanayoashiria neema kwa Tanzania yetu.
” Balozi Sefue ambaye atakumbukwa na waandishi wa habari nchini kwa kutoa ushirikiano na kujibu maswali yao muda wowote bila ubaguzi, alisema Tanzania itapiga kasi kubwa ya maendeleo akijenga juu ya yale yaliyofanywa na walio nyuma yake, lakini kasi yakuibadili Tanzania ni kubwa.
"Bila shaka Mwenyezi Mungu atatusaidia tutafanikiwa, Watanzania wote tumuombee Rais wetu aendelee kutuongoza tufikie nchi nzuri kiuchumi,” alisema.
Baada ya Balozi Sefue kuondolewa katika wadhifa huo, Rais Dk. Magufuli alimteua Balozi Mhandisi John Kijazi, kushika nafasi hiyo. Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: