Chama cha Democtratic Alliance
nchini Afrika Kusini kumeanzisha kampeni ya kumuondoa Rais Jacob Zuma
madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka
katiba.
Mahakama ilipata kuwa bwana Zuma alikataa kutii agizo
kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kamtaka alipe
pesa zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake ya kibinafsi.
Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili
kumlazimu rais Jacob Zuma kuzingatia matokeo ya uchunguzi yaliofanywa na
mkaguzi wa hesabu za serikali, kwamba alihusika na mabadiliko
yaliofanyiwa nyumba yake ya Nkandla.
Mamilioni ya madola
yalitumika katika kile kilitajwa na serikali kuwa uimarishaji wa
usalama. Marekebisho hayo yalishirikisha ukumbi,kidimbwi cha kuogelea na
zizi la ngombe
Post A Comment: