Tatizo la utoaji mimba limebainika kuwa ni kubwa hapa nchini ambapo
kwa mwaka 2013 imekadiriwa kuwa mimba 405,000 zilitolewa kwa wastani wa
kiwango cha mimba 36 kwa kila wanawake 1000 wenye umri kati ya miaka
15-49 na uwiano wa utoaji mimba 21 kwa kila watoto 100 wanaozaliwa
wakiwa hai.
Kiwango hiki kimetajwa kuwa sawa na wastani wa kiwango cha kanda ya
Afrika mashariki kwa ujumla na juu kidogo ukilinganisha na kiwango cha
nchi za Kusini mwa sahara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utoaji mimba kitaifa na
huduma baada ya kuharibika mtafiti kutoka chuo kikuu cha afya na sayansi
shirikishi Muhimbili Projestine Muganyizi amesema sheria za utoaji
mimba na mila na desturi zilizopo zina utata katika suala hili ambapo
sheria ya makosa ya jinai huidhinisha utoaji mimba ili kuokoa maisha ya
mwanamke lakini haijaweka bayana kama utaratibu huu utalinda afya ya
mwili na akili ya mwanamke huku hofu ya kushtakiwa kwa wananwake na
watoa huduma ya afya pia ikisababisha wanawake kutoa mimba kwa siri kwa
njia ambazo mara nyingi si salama na kuchangia katika vifo vya
wajawazito.
Bw. Muganyizi amesema utafiti huo umefanyika katika mikoa ya Tanzania
bara na viziwani ambapo mikoa ya kanda ya ziwa imeonyesha kuwa na
kiwango cha juu kwa asilimia 51 ikifuatiwa ni mikoa ya nyanda za juu
kusini asilimia 47, magharibi 44 huku zanzibar ikiwa na asilimia 11
ambayo ni ndogo kuliko maeneo yote.
Post A Comment: