Kampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zimeshauriwa kuhifadhi
kumbukumbu zao katika kituo cha taifa cha kuhifadhia kumbukumbu DATA
CENTRE ambacho kinatarajiwa kuanza rasmi kuhifadhi kumbukumbu mwezi Mei
mwaka huu.
Rai hiyo imetolewa na waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea kituo hicho cha Taifa cha
kuhifadhia kumbukumbu kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo
amesema itashangaza sana kwa mtanzania kwenda kuhifadhi kumbukumbu nje
ya nchi wakati tayari taifa limeshaanzisha kituo cha kisasa kwa
madhumini hayo
Profesa Mbarawa amesema katika biashara ya vituo vya kuhifadhi
kumbukumbu, kituo hicho ni kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki na
Kati.
Aidha Profesa Mbarawa amesema serikali ina mpango wa kujenga vituo
vingine viwili vya kuhifadhia kumbumbu katika mkoa wa Dodoma na Zanzibar
huku akiwahakikishia wananchi na wadau mbalimbali kuwa kumbumbuka hizo
zitahifadhiwa katika hali ya usalama bila usumbufu wowote.
Post A Comment: