ads

MFALME wa Saudi Arabia, Salman Bin Abdulaziz Al Saud amemhakikishia Rais John Magufuli, kuwa nchi yake imeichagua Tanzania kuwa nchi ya kipaumbele katika mpango wake wa kuimarisha zaidi mahusiano na Afrika uliolenga kuendeleza na kukuza biashara, uwekezaji na kushiriki katika miradi ya maendeleo.


Ujumbe wa Mfalme Salman uliwasilishwa kwa Rais Magufuli jana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Adel Al Jubeir Ikulu jijini Dar es Salaam. Katika salamu hizo pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuiongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania, Mfalme Salman Bin Abdulaziz Al Saud amesema Saudi Arabia imedhamiria kukuza zaidi mahusiano kati yake na Tanzania ili kuwaletea manufaa makubwa wananchi.

Kwa upande wake, Dk Magufuli amemshukuru Mfalme wa Saudi Arabia kwa kumtumia ujumbe na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuiongoza Tanzania na amemhakikishia kuwa Serikali yake itafurahi kuona Saudi Arabia inashirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kati na barabara.

Maeneo mengine ambayo Rais Magufuli na Waziri Adel Al Jubeir wameyazungumzia ni ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika kuendeleza elimu, utalii, bandari na miundombinu.

Pamoja na kufanya mazungumzo hayo, Rais Magufuli pia alishuhudia utiaji saini wa mkataba kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za uchumi, biashara, uwekezaji, ufundi, vijana na michezo.

Kwa upande wa Tanzania, mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, na kwa upande wa Saudi Arabia umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Adel Al Jubeir.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: