NAHODHA wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana
Samatta amesema Taifa Stars bado ina nafasi ya kufuzu fainali za Afrika
(Afcon) mwakani.
Samatta
anayecheza klabu ya KRC Genk iliyopo Ligi Kuu ya Ubelgiji, alisema
amesikia kuhusu timu ya Taifa ya Misri kushinda mchezo wake dhidi ya
Nigeria juzi na hivyo kufikisha pointi saba ambazo ndizo Tanzania
inaweza kuzifikia ikishinda michezo yake miwili iliyobaki.
“Nimesikia Misri imeshinda bao 1-0 na sasa wana pointi saba,
ukiangalia kwa juujuu unaweza kudhani wameshafuzu, lakini kiuhalisia
bado, soka haipo hivyo. “Misri watakuja Dar es Salaam tunaweza kuwafunga
kama walivyotufunga kwao (Misri iliifunga Taifa Stars mabao 3-0), pia
mechi yetu ya Nigeria tukishinda tutakuwa nasi na pointi saba,
tutashindana tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa,” alisema Samatta.
Kwa upande wake Mshauri wa Benchi la Ufundi la Taifa Stars, Abdallah
Kibadeni, amesema Stars bado ina nafasi na kwamba matokeo ya Misri
yasiwakatishe tamaa mashabiki.
Post A Comment: