WAKATI zaidi ya watu 150 wakijitokeza kuhakiki silaha zao, kutii
agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani
amesema uhakiki huo sasa unafanyika nchi nzima.
Kamishna Athumani amesema hayo jana alipozungumza na waandishi wa
habari, huku akikataa kutaja majina ya vigogo waliojitokeza kuhakiki
silaha zao kwa sababu za kiusalama.
“Baada ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kufanya uhakiki wa
silaha zake hivi karibuni, watu zaidi ya 150 wakiwemo viongozi
mbalimbali wa Serikali, viongozi wastaafu, wabunge na mabalozi wa nchi
mbalimbali wamejitokeza,” alisema.
Mbali na vigogo hao, Kamishna Athumani amesema wananchi wengine
wameonesha nia ya kufanya hivyo na kusisitiza kuwa, lengo la uhakiki wa
silaha hizo ni kuboresha hali ya usalama kwa kuwajua watumiaji .
Alifafanua kuwa utambuzi huo unafanyika kwa kuwa kunaweza kutokea
sababu mbalimbali zitakazofanya wamiliki wa awali wasiendelee kumiliki
silaha hizo, ikiwemo vifo na ulemavu.
Post A Comment: