Mbunge wa Nyamagana Jijini Mwanza Stanslaus Mabula amesema kuwa ahadi ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya
'Tanzania ya Magufuli ni ya Viwanda' ni nzuri ila aanze na vilivyokufa
kunusuru vijana ambao hawana kazi.
Mabula
ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix
kinachorushwa na EATV ambapo amesema jijini Mwanza kulikuwa na viwanda
vikubwa 7 ambavyo vilikuwa vinafanya kazi hapo awali ambapo kwa sasa
havifanyi kazi.
''Kulikuwa na viwanda 7 vya samaki ambavyo vilikuwa na uwezo wa kuajiri vijana 500 kwa siku ambapo kwa sasa vyote havifanyi kazi jambo ambalo limesababisha vijana wengi kuwa machinga katika jiji la Mwanza na maeneo mengine nchini na wengi kukosa kazi kabisa, ni vyema viwanda hivyo vifufuliwe kwanza kabla ya kuanza ujenzi wa viwanda vingine'' Amesema Mabula.
Kuhusu ahadi zake kwa wananchi Mabula amesema kuwa tatizo kubwa la maji ameshaanza kulishughulikia na miradi ya maji itaanza hivi karibuni baada ya hatua zote muhimu kukamilika.
"Tuna mradi wa Euro laki moja, nina uhakika, maeneo yote ambayo bado yana shida ya maji, hata kwenye kata yangu ya Mkolani, tatizo hilo litakwisha"
Kuhusu suala la miundombinu, Mabula amesema mkakati wake ni kuhakikisha barabara zote mbovu zinapitika kwa kiwango cha lami.

Post A Comment: