Waziri wa Maliasili na Utalii Prof JUMANNE MAGHEMBE amewasimamisha
kazi baadhi ya watendaji wakuu wa Wakala wa huduma za Misitu-TFS na
mameneja saba wa kanda wa wakala huo pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa
wanyama pori Dk Charles Mulokozi kutokana na makosa mbalimbali
yaliyoisababishia hasara serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Waziri
Maghembe amesema wakala wa Misitu Tanzania watendaji wake wameshindwa
kusimamia ipasavyo rasilimali za mazao ya misitu, na kusababisha uvunaji
holela na kupelekea kuchomwa moto kwa magogo yenye thamani ya zaidi ya
shilingi milion 500 ambayo yalitaifishwa na serikali baada kubainika
kuvunwa bila vibali.
Magogo hayo yaliyokamatwa wilayani Kalambo Mkoa wa Rukwa, yalitakiwa
kukusanywa na kupelekwa kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya, lakini TFS
walishindwa kusimamia ukusanyaji wake na hatimaye kuchomwa moto na watu
wasiojulikana.
Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii amemsimamisha
kazi Dk. Charles Mulokozi ambaye alikuwa Mkurugenzi Msaidizi wa
Matumizi Endelevu ya Wanyamapori baada ya kubainika kutoa vibali vya
kusafirisha nyani 61 licha ya kwamba alikataliwa kutoa vibali hivyo.
Kwa mujibu wa Prof Maghembe alipata taarifa za kundi la watu ambalo
lilikuwa likikusanya nyani kutoka mapori na hifadhi mbalimbali ambapo
nyani 450 walibainika kukusanywa na hivyo kuamua kuzuia vibali vyote vya
kusafirisha wanyama lakini Dk Mulokozi aliamua kutoa kibali cha
kusafirisha nyani hao kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.
Akitangaza hatua zilizochukuliwa dhidi ya nyani hao ambao walikuwa wakisafirishwa kwenda nchi za Ulaya Mashariki,
Post A Comment: