GWIJI wa soka Ulaya na Duniani kwa Ujumla Johan Cruyff(68) amefariki dunia leo hii kwa maradhi ya kansa.
Cruyff aliyewahi kuzichezea klabu za Barcelona na Ajax kwa vipindi tofauti amefikwa na umauti huo huku dunia ya soka ikimkumbuka kwa mchango wake mkubwa alioutoa wa kubadili mchezo wa soka.
Gwiji huyo ambaye pia alitamba na timu ya taifa ya Uholanzi kama mchezaji na baadaye kocha katika vilabu vya Ajax na Barcelona anakumbuka kuwa miongoni mwa watu wa awali kubuni na kuanzisha mradi wa kituo cha soka cha Barcelona La Masia na kile cha Ajax.
Katika kipindi cha uhai wake Cruyff alifanikiwa pia kuiongoza Barcelona kutwaa taji la kwanza la michuano ya klabu bingwa ulaya akiwa kama kocha mwaka 1992.
Pia aliongoza Barcelona kushinda ubingwa wa Hispania mara nne mfululizo katika msimu wa mwaka 1990 -1994
Aidha Cruyff ambaye pia aliwahi kudhuru nchini Tanzania,anakumbukwa kama mwanzilishi wa soka la pasi fupifupi dunaini ambapo alifanya hivyo alivyokuwa katika klabu ya Barcelona.
Post A Comment: