Rais wa Marekani Barack Obama
ameeleza matumaini yake kwamba hali ya Cuba itaimarika, kwenye hotuba
iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga.
Kiongozi huyo wa
Marekani, ambaye ndiye wa kwanza kuzuru Cuba akiwa bado madarakani
katika kipindi cha miaka 88, alitoa hotuba hiyo kutoka ukumbi wa Grand
Theatre mjini Havana.
Bw Obama alisema alifika Cuba “kuzika masalio ya Vita Baridi” na miongo mingi ya uhasama.
Alimwambia Rais wa Cuba Raul Castro kwamba hafai kuiogopa Marekani na pia hafai kuogopa “usemi wa watu wa Cuba
Bw Obama alisema wakati umefika kwa Marekani na Cuba kuacha nyuma
yaliyopita na kusonga mbele
Amewataka raia wa Cuba kuacha nyuma vita vya kifalsafa na kujieleza
sio kwa kupinga Marekani bali kwa kujieleza wao binafsi ama raia wa
Cuba.
"Licha ya siasa hizi zote, watu ni wale wale na Wacuba ni Wacuba,” alisema.
Aidha,
amehimiza kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara vilivyowekewa nchi hiyo
na Marekani miaka 54 iliyopita. Tamko hilo lilishangiliwa sana na raia
wa Cuba.
Ni Bunge la Congress pekee linaloweza kuidhinisha kuondolewa kwa vikwazo hivyo.
Bw
Obama alikamilisha ziara yake ya siku tatu kwa kuungana na Rais Castro
kutazama mechi ya besiboli uwanja wa Latinoamericano mjini Havana.
“kama marafiki na majirani na kama familia,
pamoja” kwa siku za usoni zenye ufanisi.
Post A Comment: