Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umetishia kujitoa katika ushiriki
wa Ligi kuu soka Tanzania bara endapo Shirikisho la soka nchini Tanzania
TFF litaendelea hatu a za kutojibu na kutoshughulikia malalamiko yao
mbalimbali waliyowapelekea.
Suala hilo limekuja baada ya klabu hiyo kuiandikia barua TFF ya
kulalamikia kuvurugika kwa ratiba ya ligi kuu soka Tanzania bara hasa
madai ya kuwepo kwa viporo vingi kwa klabu za Yanga na Azam Fc ambazo
zinashiriki mashindano ya kimataifa hivi sasa.
Akizungumza mara baada ya kupeleka barua ya kulalamikia madai hayo
katika makao makuu ya TFF yaliyopo karume jijini Dar es Salaam, Mkuu wa
Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara amesema wameamua
kufanya hivyo baada ya kuona mara nyingi TFF ikisena haijapokea barua
kutoka kwao.
Manara amesema barua yao kwenda kwenye kwenye Wizara ya Habari,
Utamaduni, Wasanii na Michezo wameitaka TFF kuanza kufanyia kazi
malamiko yao na kufatilia Kesi zote walizowapeleka ikiwemo kesi ya
Ramadhani Singano kuelekea Azam fc,kesi ya Mshambuliaji wa Yanga Donald
Ngoma kumpiga kichwa mchezaji wao Hassan Kessy,kesi ya Mkuu wa kitengo
cha habari na mawasiliano cha klabu ya Yanga Jerry Muro kutoa maneno ya
kibaguzi dhidi ya klabu ya Simba.
Post A Comment: