Sara Kaisi ‘Shaa’ ni miongoni mwa Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya
anayekerwa na hatua ya kutoelewana kwa nyota wawili wa muziki huo
Diamond na Ali Kiba na sasa anapata wakati mgumu anaposikia uhasama huo.
Alisema kuwa umefika wakati sasa vyombo vya habari kuacha kukuza
uhamasa huo,kwa madai kwamba ndivyo vilivyotengeneza bifu kwa kuleta
hizo timu zilizosababisha matatizo makubwa kwenye muziki wa kizazi kipya
nchini.
”Sio mashabiki pekee wanaokerwa na kutoelewana kwa wasanii wawili
wakubwa hata mimi ninakerwa na hali hiyo hasa kwa kuzingatia kwamba wote
ninawapenda na kuheshimu kazi zao,”alisema Shaa na kuendeleza.
”Niseme kwamba bifu hilo linaniweka katika wakati mgumu kwani kama
nilivyosema,wasanii wote wawili ninawapenda na kukubali sana kazi
zao,hivyo ni muhimu likaisha haraka kwa sababu halina faida.”
Post A Comment: