ads

Mkali wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki, amesema hawezi kusahau mwaka 2015 kwa kuwa ni mwaka ambao alikuwa na ‘mzuka’ wa ajabu wa kazi tofauti na mwaka huu.

Akizungumza na Timesfm Roma amedai kuna uwezekano kabisa mwaka huu asirekodi wimbo wowote ule. “Nilifanya kazi nyingi mwaka 2015 na nilikuwa na mzuka wa ajabu, yani naweza mwaka huu (2016) nisirekodi kabisa. “Kazi yangu inakuwa ni kuanza kuziachia tu” Alisema Roma

Licha ya hayo Roma kwa sasa anatamba na wimbo wa Mtoto wa Kigogo aliomshirikisha staa wa shindano la kusaka vipaji Bongo Star Search BSS Walter Chilambo, huku akitamba na ngoma nyingine aliyo shirikishwa na rapa Baghdad inayoitwa Una Akili wewe?

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: