Hatimaye Bodi ya Ligi (TPLB) inayosimamia ligi za soka nchini imefanya mabadiliko katika ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ratiba inayozingatia usawa, haki na inayopunguza kwa sehemu kubwa
mnyukano wa viporo uliolundikwa pasi na sababu kwa klabu za Yanga na
Azam.
Tunaamini mabadiliko hayo yatarudisha walau imani ilioanza kupotea
kwa bodi na TFF toka kwa wapenzi, mashabiki na wanachama wa Simba.
Hakika viporo vile vilikuwa na taswira isiyopendeza kwa afya ya ligi na mchezo wenyewe wa soka nchini.
Sasa kwa spirit ile ile ya bodi na uharaka ule ule tunaamini TFF nao watashughulikia malalamiko mengine tuliowasilishia kwao.
Tunachokitaka kwa wakubwa hawa sio kupendelewa bali kupewa haki na sio kwa Simba tu, pia kwa klabu nyingine zote nchini.
Nawaomba wanachama na washabiki wetu mtuunge mkono katika mapambano haya mazito tunayoendelea nayo.
Mwisho kwa niaba ya Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva, wajumbe wa
kamati ya utendaji, sekretarieti, benchi la ufundi na wachezaji,
tunawatakia furaha na baraka tele kuelekea kwenye sikukuu za Ijumaa Kuu
na Pasaka.
Tunawapenda sana.
Simba Nguvu Moja
De la boss
Haji Manara
Post A Comment: