ads

Msemaji wa Chama cha Mapinduzi Christopher Ole Sendeka amesema CCM ni chama ambacho ni kimbilio la wanyonge wanapopata shida katika jamiii tokea zamani.


Ole Sendeka ameyasema hayo wilayani Simanjiro aliposhiriki zoezi la kuwaingiza kazini viongozi wa kimila wa kabila la wamasai.

''CCM ni kimbilio la wanyonge hivyo nawataka viongozi wa CCM kila mtu kwenye eneo lake kuhakikisha anasikiliza na kutatua kero za wananchi ili kuhakikisha chama hicho kinarudisha imani yake yote kwa wananchi kama ilivyoliwa zamani''-Ole Sendeka.

Naye mwenyekiti wa CCM wilayani Simanjiro Brown Ole Suya amesema chama hicho kinaacha mchakato wa kuwashuhulikia watu wote waliopo kwenye chama ambao walikisaliti chama hicho kipindi cha uchaguzi.

Aidha mwakilishi wa viongozi hao wa kimila Christopher Kuya amesema wameanza kurudisha imani na Chama Cha Mapinduzi kutokana na kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya tano hasa utumbuaji wa majipu.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: