Meneja mpya wa klabu ya Man City, Pep Guardiola, amedhamiria kukifuma
upya kikosi cha klabu hiyo kwa kumjumuisha kiungo kutoka nchini
Ufaransa na klabu bingwa nchini Italia, Juventus Paul Pogba.
Guardiola ambaye ataanza kazi huko Etihad Stadium, mwishoni mwa msimu
huu, amedhamiria kufanya hivyo kwa lengo la kujenga kikosi kitakachokua
na ushindani wakati wote, na hatimae kufikia lengo la kutwaa mataji
makubwa nchini England pamoja na barani Ulaya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Hispania, imeelezwa kwamba meneja
huyo ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha FC Barcelona amepnga kuanza
kufanya usajili wa kumuhamisha Pogba kutoka nchini Italia.
Hata hivyo huenda akapata wakati mgumu katika zoezi hilo, kutokana na
klabu nyingine kama Chelsea, PSG na Real Madrid kuwa katika mipango ya
kumuwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23.
PSG wameripotiwa kutenga kiasi kikubwa cha pesa kama ada ya uhamisho
wa Pogba, itakapofika mwishoni mwa msimu huu, kutokana na hitaji la
mchezaji mwenye kujituma walilonalo kwa sasa, kutokana na Zlatan
Ibrahimovic, kuwa mbioni kuondoka.
Wakati ikielezwa hivyo Guardiola, anajiaminisha kwamba mwenyekiti wa
klabu ya Man City, Khaldoon Al Mubarak atakua na kila sababu ya
kupambana na mipango hiyo ya klabu pinzani na itakapotokea dau la
usajili wa Pogba kupanda, matajiri hao wa mjini Manchester hawatoshindwa
kupambana hadi mwisho.
City wanatajwa kutenga kiasi cha pauni million 71, kama ada ya
usajili wa Pogba, lakini wamejipanga kuanza kuwasilisha ofa ya paund
million 60 huko Juventus Stadium
Post A Comment: