Kiongozi wa pili kwa ukubwa katika
itifaki ya kundi la wapiganaji la Islamic State ameuawa katika
oparesheni iliotekelezwa na Marekani nchini Syria mwezi huu, vyombo vya
habari vya Marekani vimesema.
Maafisa wa ulinzi wameliambia
shirika la habari la NBC kwamba Abdul Rahman Mustafa al- Qaduli,raia wa
Iraq anayejulikana kama Hajji Iman aliuwawa katika uvamizi mwezi huu.
Waziri
wa maswala ya ulinzi nchini Marekani Ash Carter alitarajiwa
kuthibitisha kifo cha mwana jihad huyo na kutoa maelezo ya uvamizi huo.
Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya dola milioni saba kwa mtu yeyote ambaye angetoa habari za Qaduli.
Qaduli alizaliwa mwaka 1957 ama 1959 kaskazini mwa mji wa Iraq wa Mosul ambao ulidhibitiwa na IS tangu mwaka 2014.
Alijiunga
na al-Qaeda nchini Iraq mwaka 2004 chini ya uongozi wa marehemu Abu
Musab al-Zarqawi akihudumu kama naibu wake na kiongozi wa eneo la Mosul
kulingana na Marekani.
Baada ya kuachiliwa kutoka kwa jela za Iraq mapema mwaka 2012,alijiunga na vikosi vya IS nchini Syria.
CHANZO- BBC
Post A Comment: