ads

Klabu ya Leicester City ya Uingereza itacheza dhidi ya miamba wa Ulaya, klabu ya Barcelona kutoka Uhispania, Agosti mwaka huu.


Klabu hizo zitakutana katika michuano  ya Kombe la Mabingwa wa Kimataifa ambalo huchezwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Viongozi hao wa Ligi ya Uingereza pia watakutana na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain.Leicester watakutana na Celtic mjini Glasgow tarehe 23 Julai, PSG mjini Los Angeles tarehe 30 Julai na Barcelona mjini Stockholm tarehe 3 Agosti.

Klabu hiyo ni miongoni mwa klabu tano za Ligi ya Uingereza zitakazoshiriki michuano hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa huchezewa Marekani.

Klabu nyingine kutoka Uingereza ni Manchester United, Liverpool, Manchester City na Tottenham Hotspur.

Msimu mpya wa Ligi ya Premia utaanza Jumamosi tarehe 13 Agosti.

Ratiba ya Mechi za Klabu Bingwa Kimataifa
  • 23 Julai - Celtic v Leicester, Glasgow
  • 24 Julai - Inter v PSG, Eugene
  • 27 Julai - Real Madrid v PSG, Columbus
  • 27 Julai - Bayern Munich v AC Milan, Chicago
  • 27 Julai - Chelsea v Liverpool, Pasadena
  • 30 Julai - Celtic v Barcelona, Dublin
  • 30 Julai - Inter v Bayern Munich, Charlotte
  • 30 Julai - AC Milan v Liverpool, Santa Clara
  • 30 Julai - PSG v Leicester, LA
  • 3 Agosti - Barcelona v Leicester, Stockholm
  • 3 Agosti - Bayern Munich v Real Madrid, East Rutherford
  • 3 Agosti - AC Milan v Chelsea, Minnapolis
  • (Kuthibitishwa baadaye) - Liverpool v Barcelona
  • (Kuthibitishwa baadaye) - Inter v Celtic
  • (Kuthibitishwa baadaye) - Real Madrid v Chelsea
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: