Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli
ametoa zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni tisa laki
tatu na elfu sabini kwa vituo 24 vya kulelea watoto yatima na wazee
wasiojiweza nchini kwa lengo la kuungana nao katika kusheherekea sikukuu
ya Pasaka.
Msaada huo uliotolewa na Rais ni pamoja na Mchele, Mbuzi na mafuta ya
kupikia ambao utakwenda kwenye vituo 6 vya watoto yatima vilivyoko
jijini jijini Dar es salaa, na vituo viwili vya Zanzibar, Tabora,
Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Kagerai na Morogoro na kituo kimoja kwa
mikoa Tanga, Ruvuma, Shinyanga, Mtwara na Mara.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Rais kwa wafanyakazi wa vituo
hivyo Kamishna wa Ustawi wa Jamii Rabikila Mushi amesema kuwa msaada huo
uliotolewa na Rais Magufuli ni moja ya utaratibu wa kawaida wa Marais
tangu awau nne zilizopita kuwapatia zawadi makundi maalum vyakula ili
kuwawewezesha kufurahi na kusherehekea sikukuu mbalimbali kama wananchi
wengine wa kawaida katika jamii.
Post A Comment: