Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Ali Mohamed Sein ameahidi Serikali yake mpya atakayoiunda itafuata Misingi ya Haki na Uadilifu na hakuna mtu atakayebaguliwa .
Dkt.Shein pia ame ahidi kuwa Seriklai yake itashirkiana na vyama vya siasa vya upinzani katika kujenga serikali mpya .
Hiyo itahusu zaidi utekelezaji wa Ilani ya chama chake cha
Mapinduzi yenye vipenge vinne vya ajira,mapambano dhidi ya
umaskini,rushwa na kulinda umoja wa kitaifa.
Ameyasema hayo baada ya kuapishwa kuwa kiongozi wa Zanzibar kwa awamu ya saba kipindi cha pili.
Wakati wa kuapishwa dua zilizosomwa na viongozi wa dini wa
madhehebu mbali kabla ya kupanda kwenye jukwa kupokea salamu za rais na
kupandishwa kwa bendera ya rais.
Baadaye alikagua Gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na
majeshi ya ulinzi na usalama kabla ya kutoa hotuba yake kuhusu awamu ya
pili ya uongozi wake.
Miongoni mwa waliohudhuria sherehe ya kuapishwa kwake kwenye Uwanja
wa Aman Zanzibar ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John
Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu,Kassim
Majaliwa na viongozi mbalimbali wastaafu.
Post A Comment: