Star wa Bongo flava, Juma Nature, ameendelea kusisitiza kuwa
anahitaji kwa ‘udi na uvumba’ pambano la kimuziki kati yake na Naseeb
‘Diamond’ Abdul ili kuinua tasnia ya muziki hapa nchini.
Akizungumza , Nature amedai kuwa yeye ndiye mpinzani
pekee wa Diamond kwa sasa na asinukuliwe tofauti hana chuki yoyote na
Plutnumz zaidi ni kwa maslahi ya Bongo Flava pekee.
“Watu wanamtukuza sawa lakini watuweke stage moja tuone nani
atakamua, unajua tuseme ukweli Bongo Flava sasa mimi na Diamond ndio
wapinzani pekee.
“Watu waandae pambano, na mpunga pia uwepo nioneshe na mimi nguvu yangu ilivyo mtaani” Alisema.
Katika ‘line’ nyingine, Kiroboto amefunguka pia aina ya mziki
waliokuwa wanafanya zamani ndio ilikuwa kitambulisho pekee cha Bongo
Flava tofauti na sasa wasanii wengi wanaiga aina ya mataifa mengine.
Post A Comment: