Msanii wa Bongo Fleva nchini Judith Wambura a.k.a Lady Jay dee amesema
yeye kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa wimbo siyo kwamba alifulia
bali aliamua kutotoa wimbo kwa malengo.
Jaydee ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV kuhusiana na yeye
kukaa muda mrefu kabla ya juzi kuachia ngoma mpya aliyoipa jina la ‘Ndi
Ndi Ndi’
”Kupotea ni tofauti na mtu aliyelala na kuamka, mimi nime ‘maintain’
niliamua kutotoa wimbo na niliposema naamka tena watu walidhani ndiyo
jina la wimbo lakini haikuwa malengo hayo”-Amesema Jaydee.
Aidha Msanii huyo amesisitiza kuwa kutoa wimbo siyo tuu kutoa kwa
sababu watu wanatoa bali msanii anatakiwa kutumia akili na kutokurupuka
katika kutoa wimbo.
Post A Comment: