ads

Rapa mkongwe nchini Jay Mo amefunguka kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa suala la vyombo vya habari kuanza kuwalipa wasanii(mirabaha) siyo jambo ambalo linapaswa kuchukuliwa kama msaada hata kidogo kumfanya msanii adumu au atoboe kwenye game.

Jay Mo amesema hata wasanii wakilipwa au wasipolipwa bado kipaji cha mtu ndicho kitakachomfanya afanikiwe kwenye tasnia ya muziki lakini mirabaha siyo njia ya wasanii waliokwama kwenye game kutoka.

Amejaribu kuonyesha utofauti uliopo kwa wale wanaodhani kuna wasanii wanaoweza kufanikiwa kwenye game endapo mirabaha itaanza kulipwa akisema msanii mkali na mwenye kipaji cha kweli pekee ndiye atakaye toboa bila kujali atalipwa mirabaha au hatolipwa.


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: