ads

Ukiachilia mbali aliposikika kwenye Like Father Like Son Remix ya msanii Stamina ni muda mrefu umepita hajasikika Noorah, huku wengi wakijiuliza nini sababu za ukimya wa msanii huyo.

Kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio Noorah ameeleza kuwa ukimya wake ni kuhofia kutoa ngoma ambayo haitofanya vizuri, pia hapendi kukurupuka kutoa ngoma kuwepo mipango maalum kuhusu ngoma hiyo.

Noorah amesema kuna ngoma kadhaa kali aliwahi kuzitoa siku za nyuma lakini mipango ya promo haiku na kusababisha ngoma hizo kupotea kiaina jambo ambalo hataki litokee tena kwa ngoma zijazo.

Ameweka wazi kuwa zipo ngoma kibao ambazo amerekodi tayari lakini mipango ya Promo haijaridhisha kwahiyo anaona bora kukaa kimya kuliko kuzitoa hovyo zikapotea.


 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: