SAKATA la kukamatwa kwa tumbili waliokuwa mbioni kusafirishwa nje ya
nchi, limechukua sura mpya baada ya idadi ya waliokamatwa mpaka sasa
kufikia watu saba wakiwemo maofisa wanne wa serikali.
Miongoni mwa waliokamatwa ni Ofisa Mfawidhi Kanda ya Kaskazini
anayehusika na Matumizi Endelevu ya Wanyamapori nchini Nyangabo Musika,
Idd Misanya anayedaiwa kuwauzia wanyama hao.
Akizungumza , Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa aliwataja watu hao kuwa ni Juma Eliasa
ambaye ni Mkurugenzi wa Manyara Bird wakiunganishwa na raia wa Uholanzi
waliokamatwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA, Arten Vardanian (52) na Edward Vardanian (46).
“Tumewakamata watu hawa na bado tunaendelea na mahojiano zaidi,
uchunguzi utakapokamilika tutawafikisha mahakamani,” alisema Kamanda
Mtafungwa.
Wakati kamatakamata hiyo ikiendelea, wafanyabiashara wanaohusika na
uwindaji wa wanyama hao wanalalamikia kitendo cha kukamatwa kwa wageni
hao kuwa kitaathiri biashara yao hiyo.
Post A Comment: