Pamoja na mashabiki wengi wa soka nchini kuonekana wana hofu kubwa na Al Ahly, wao pia wameonekana kuwa na hofu kubwa na Yanga.
Kikundi cha mashabiki wa Al Alhy maarufu kama Ultras kimekuwa kikijadili wachezaji wa Yanga kupitia mitandao mablimbali ya mashabiki hao.
Amissi Tambwe amekuwa gumzo ingawa wamekosea baada ya kusema ndiye anayeongoza kwa upachikaji mabao.
Mashabiki hao wanajaribu kuangalia namna ambavyo safu ya ulinzi inavyoweza kumzuia kwa kuwa anaonekana ni hatari.
Mashabiki wengine wamezungumzia kuhusiana na Tambwe, alivyoibuka mfungaji bora wa Kagame Cup kabla ya kuja Tanzania alipokuwa akiichezea Vital’O ya Burundi.
Wako ambao wamekuwa na imani na kikosi chao na wale ambao wana hofu na mshambuliaji huyo huku wakitolea mfano wa makosa kadhaa ambayo yamekuwa yakifanywa na safu yao ya ulinzi.

CREDIT-SALEH JEMBE
Post A Comment: