Serikali ya mkoa wa Mtwara imelazimika kuimarisha ulinzi katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula baada ya Daktari
aliyefahamika kwa jina la Dikson Saini kupigwa na kudhalilishwa na ndugu
wa mgonjwa baada ya kutoa Rufaa ya kwenda kutibiwa Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili kutokana na tatizo lake la kuvunjika taya kushindikana
katika hospitali hiyo.
Akizungumzia tukio hilo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara
aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa kwenye kikao cha Madaktari ambao mara baada
ya tukio hilo walisimama kazi kwa muda wakitaka ufumbuzi wa suala hilo
kwa Serikali ya mkoa.
Kwa hisia baadhi ya madaktari wamelaani kitendo hicho na kutaka
serikali ichukue hatua staiki vinginevyo watashindwa kufanya kazi iwapo
wataendelea kudhalilishwa.
Hata hivyo kwa hatua nyingine ndugu hao wa mgonjwa walihoji iweje
Hospitali ipokee fedha za kumuona daktari,vipimo vya X-ray,na kitanda
wakati walijua hawawezi kumtibu mgonjwa wao,ambapo baada ya tukio hilo
walimtorosha mgonjwa na wenyewe kutoweka.
Post A Comment: