KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars Charles Mkwasa
amesema kitendo cha Chad kujitoa kwenye michuano ya Afrika
kimemnyong’onyesha. Chad iliyokuwa icheze mechi ya marudiano ya kuwania
kufuzu kwa fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) 2017
dhidi ya Stars jana, ilitangaza kujitoa kutokana na ukata.
Akizungumza , Mkwasa alisema timu yake ilishajiandaa kushinda
mechi ya jana na kwamba wachezaji walikuwa kwenye ari kubwa. Katika
mechi ya kwanza iliyochezwa mjini N’Djamena Jumatano iliyopita, Stars
ilishinda bao 1-0 na kufufua matumaini kwenye michuano hiyo.
“Baada ya ushindi ule wachezaji wangu walikuwa kwenye ari kubwa na
walikuwa na uhakika wa kushinda mechi ya marudiano, lakini jambo la
kujitoa kwa wapinzani wetu limetunyong’onyesha wote,” alisema.
Aidha Mkwasa alilaumu kwamba vitendo kama jivyo ndivyo
vinavyosababisha soka ya Afrika haipigi hatua kwa baadhi ya nchi
kutokana na kutokuwa makini. “Soka ya Afrika kwa baadhi ya nchi haiwezi
kwenda mbele zaidi, hili linakatisha sana tamaa hatuna tu la kufanya,”
alisema.
Post A Comment: