Baraza la sanaa Tanzania wenye jukumu la kusimamia Sanaa na kuratibu
Burudani, BASATA, wamepiga marufuku disco toto katika kumbi za starehe.
Hii ni taarifa rasmi:
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa
na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za
burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali
vyao vya uendeshaji wa kumbi.

Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa
kumbi zao, kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi, kuepuka kelele
zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha
ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.

Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za sherehe na
burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia
kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ katika msimu huu wa Sikukuu ya Pasaka ili
kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi
wamekuwa wakijisahau na kuendekeza faida katika biashara zao kiasi cha
kuandaa madisko ya watoto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa ambayo
yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa kumbi kwa msingi huohuo wa
kuendekeza faida pasi na kujali maelekezo ya vibali vyao wamekuwa
wakijaza watu kupita viwango vya madaraja waliyopangiwa na BASATA.

BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi za sherehe na burudani
linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka
maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha
utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za
kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.

BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa Sanaa Pasaka njema na yenye
furaha tele.
furaha tele.
Post A Comment: